Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba akizungumza leo tarehe 7 Juni 2021 bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2021/22
Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa hadi Aprili 2021, madai ya jumla ya Sh965.1 bilioni yamekaguliwa na kulipwa.
Dk Mwigulu amesema hayo leo Juni 7 2021 bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake ya mwaka 2021/22.
Alisema kati ya fedha hizo, madai ya wakandarasi ni Sh704.5 bilioni, wazabuni Sh21.6 bilioni, wafanyakazi Sh97 bilioni, madeni mengine Sh92.1 bilioni, watoa huduma Sh34.2 bilioni na fidia kwa wananchi wakiahidi utekelezaji wa miradi mbalimbali Sh15.7 bilioni.
Comments
Post a Comment